Mahakama yamng’atua mamlakani rais wa Korea Kusini

Mahakama ya juu nchini Korea Kusini imeunga mkono uamuzi wa bunge wa kumuondoa rais wa taifa hilo Park Geun-hye mamlakani.

Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.

Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.

Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.

Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.

Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.

Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.within sixty days.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*