Mbowe mikononi mwa Polisi Dar

Imeandikwa na Lucy Lyatuu, Gloria Tesha na Francisca Emmanuel

KATIKA kile kinachoelezwa kuwa ni kuitikia mwito wa Jeshi la Polisi uliomtaka afike Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa mahojiano jana, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, hatimaye jana amefika kituoni hapo.

Hata hivyo, baadhi ya taarifa za viongozi mbalimbali wa chama hicho kupitia akaunti zao za mitandao mbalimbali ya kijamii na kwa njia ya simu, walipishana maelezo, wengine wakidai Mbowe amekamatwa na Polisi na wengine walisema ameamua kwenda mwenyewe Polisi.

Mnadhimu wa Chadema, Tundu Lissu katika akauti yake ya Twitter aliandika jana kuwa, Mbowe amekamatwa na Polisi.

Wakati akaunti ya Lissu ikieleza hayo, akaunti ya Facebook ya Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo ilieleza kuwa Mbowe ameamua mwenyewe kwenda Kituo Kikuu cha Polisi baada ya kuwepo taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa anahitajika polisi.

Taarifa kama hiyo ya Mbowe kuamua kwenda mwenyewe Polisi pia ilisambazwa jana kwa simu saa 9:30 alasiri na Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.

Hali ilivyokuwa Central Baada ya taarifa za Mbowe kukamatwa na nyingine zikieleza ameamua kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, gazeti hili lilifika kupata taarifa zaidi.

HabariLeo likiwa eneo la tukio, alasiri hiyo, lilifika katika meza ya maulizo ya Polisi, lakini kabla ya kuuliza chochote, askari mmoja alitaka kujua mwandishi ni nani na alipojitambulisha, alimweleza kuwa waandishi hawatakiwi eneo hilo na kumuelekeza waliko waandishi wengine nje ya kituo hicho.

Hata hivyo, askari huyo alipoulizwa kama taarifa za kuwepo Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema) ni za kweli, alimhakikishia mwandishi kuwa ni kweli Mbowe yupo kituoni hapo, lakini aliko haruhusiwi mtu yeyote kwenda.

“Ni kweli Mbowe kafika, yupo huko juu ila hakuna anayeruhusiwa kwenda,” alisema askari huyo na kumtaka mwandishi aondoke kuwafuata waandishi wenzake alikomuelekeza, nje ya kituo upande wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

Gazeti hili lilishuhudia nje ya kituo ulinzi ukiwa umeimarishwa huku askari wawili waliokuwa na silaha wakiwaondoa watu wakiwemo waandishi mpaka eneo la kukata tiketi za TRL na kuwasogeza katika eneo la ofisi.

Askari walionekana kutanda pande zote za kituo hicho cha Polisi. Saa 11:30 jioni, gazeti hili liliona gari lenye rangi ya maziwa, lenye namba za usajili T 886 BWX Toyota Land Cruiser limesimama upande wa nyuma wa kituo hicho cha Polisi, milango ikafunguliwa na kwa haraka watu kadhaa wakaharakishwa kuingizwa kwenye gari kwa sekunde chache na milango ikafungwa.

Mmoja wa watu waliokuwa eneo hilo walidai gari hilo ndilo liliwabeba Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji hivi karibuni walipofika kwa mahojiano kituoni hapo.

Hata hivyo, kwa dakika nane kutoka saa 11:30 hadi 11:38, waandishi wakijaribu kuzunguka nyuma kwa mbali kuangalia kulikoni, gari hilo lenye vyoo vya giza (tinted) liliondoka kwa kasi na baadaye ulinzi ukawa haupo tena, na hali ikarejea kawaida.

Kauli ya Kamanda Sirro Baada ya gari hiyo kuondoka, gazeti hili lilimpigia simu Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ambaye hivi karibuni alikaririwa akimtaka Mbowe kufika kituoni hapo ndani ya saa 48 zilizoisha jana kwa ajili ya mahojiano kuhusu dawa za kulevya.

Mbowe alitajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika orodha ya watu 65 Februari 8, mwaka huu, katika mkutano na waandishi wa habari akimtaka kufika Kituo Kikuu cha Polisi Ijumaa, Februari 10, mwaka huu kwa mahojiano kuhusisha na masuala ya dawa za kulevya.

Wengine waliotajwa ni Manji na Gwajima ambao wao walikwenda Polisi Alhamisi, Februari 9.

Simu ya mkononi ya Kamanda Sirro jana alipopigiwa saa 12:04 jioni ilipokewa na msaidizi wake na kueleza kuwa kamanda huyo yupo kwenye mkutano na hawezi kuzungumza na mtu kwa wakati huo.

Alipoelezwa anachotafutiwa, msaidizi huyo wa Kamanda Sirro alimtaka mwandishi ampigie kamanda baada ya saa mbili ndio atakuwa amemaliza kikao.

Mbowe kukaguliwa nyumbani? Baadhi ya maofisa wa polisi waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina, walidai Mbowe amepelekwa nyumbani kwake ili Polisi wakakague.

Makene alipotafutwa tena jana jioni, alisema hajui kinachoendelea na yupo njiani kuelekea eneo ambako atapata taarifa kuhusu nini kinaendelea.

Mmoja wa mawakili wa Chadema, Peter Kibatala alipopigiwa simu kueleza kinachoendelea, hakupokea na kutuma ujumbe mfupi kuwa atafutwe baadaye na alipotafutwa hakupatikana.

Vita ya dawa za kulevya imeongezwa nguvu na Rais John Magufuli ambaye ametangaza rasmi kuwa serikali haitamuonea mtu katika kuwasaka wasafirishaji, wauzaji na watumiaji wa dawa hizo, isipokuwa itahakikisha kila mhusika ametiwa nguvuni.

Kwa kuhakikisha hilo, wiki iliyopita Rais Magufuli alimteua na kumwapisha Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rodgers Siyanga kwa mujibu wa sheria na tayari amenza kazi kwa kueleza bayana hakuna jiwe juu ya jiwe litakalosalia katika vita hiyo.

Makonda, Sirro waitwa kortini Wakati huo huo, kutokana na sakata la dawa za kulevya linalotikisa nchi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZPC), Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO), Camilius Wambura, wamepelekewa barua za mwito za kuwataka wafike Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.

Viongozi hao wamepelekewa mwito huo kutokana na kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe dhidi yao.

Mbowe alifungua kesi hiyo kutokana na hatua ya RC Makonda kumtaja katika orodha yake ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na dawa za kulevya katika awamu ya pili na kumtaka afike katika Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 10 mwaka huu, kwa ajili ya mahojiano.

Katika kesi hiyo Namba Moja ya Mwaka 2017, Mbowe pamoja na mambo mengine, anapinga mamlaka ya RC kumkamata kwa kile anachokiita kudhalilisha watu.

Kesi hiyo imepangwa kutajwa leo na itasikilizwa na jopo la majaji watatu, Sekieti Kihiyo ambaye ni kiongozi wa jopo hilo, akisaidiana na Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Kaday.

Mbowe anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa vifungu vya Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa vinavyowapa mamlaka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwakamata watu na kuwatia mbaroni viko kinyume cha Katiba.

Aidha, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, jana alifungua maombi mahakamani hapo akipinga kusudio la Kamanda Sirro la kumkamata kama hatajisalimisha katika kituo cha polisi kwa mahojiano.

Mahakama hiyo imetoa hati za mwito wa kufika mahakamani hapo kwa wadaiwa hao ambao ni Makonda, Sirro na Wambura.

Hata hivyo, inadaiwa Kamanda Sirro alikataa kupokea mwito huo akielekeza kuwa hati hiyo ya mwito ipelekwe kwa Wambura.

Wadaiwa kukataa kusaini Kwa mujibu wa Ofisa wa mahakama, Yusuph Juma ambaye alipeleka mwito huo, alidai kuwa baada ya kuelekezwa na Kamanda Sirro kuwa ampelekee mwito huo Wambura, alipokwenda kwa Wambura, hakumkuta.

Juma alidai hati ya mwito wa mkuu wa mkoa alipoupeleka hakumkuta na kwamba wasaidizi wake nao walikataa kuusaini mwito huo.

Mwishoni mwa wiki, Kamanda Sirro akizungumza na waandishi wa habari alimtaka Mbowe ajisalimishe mwenyewe kituo cha Polisi na kwamba kama hatafanya hivyo basi watamsaka popote alipo na kumtia mbaroni.

Katika maombi hayo, Mbowe anaiomba mahakama iwazuie wadaiwa kutekeleza azma yake ya kumtia mbaroni pamoja na mambo mengine akidai kuwa kuna kesi ya kikatiba ambayo tayari ameifungua mahakamani hapo.

Katika maombi hayo, Mbowe anaiomba mahakama hiyo pia itoe amri ya kuwazuia kumkamata hadi hapo kesi hiyo ya kikatiba itakapomalizika na kwamba Mahakama Kuu imwachie na polisi wasiendelee na mchakato wowote dhidi yake hadi hapo kesi hiyo itakapomalizika.

Anachopinga Mbowe Katika kesi ya Msingi ya Kikatiba, Mbowe anapinga kitendo cha Polisi kumtaka afike kituoni kwa madai kuwa ni utekelezaji wa amri ya Mkuu wa Mkoa.

Anadai kuwa sheria inayompa Mkuu wa Mkoa mamlaka ya kutoa amri ya kumkamata na kumweka ndani mtu iko kinyume cha Katiba kwa madai kuwa ilitungwa katika mazingira ambayo hapakuwa na vituo vya polisi vya kutosha.

Anadai kuwa kwa mazingira ya sasa sheria hiyo imeshapitwa na wakati na anaiomba mahakama itamke kuwa ni kinyume cha Katiba. Mbowe pia anadai kuwa hata kama Mkuu wa Mkoa alikuwa anatekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa sheria hiyo, basi hakutimiza matakwa ya kisheria, ambayo ni pamoja na kutoa taarifa kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi.

Vile vile, anaiomba mahakama kama itaona kuwa Mkuu wa Mkoa alikuwa sawa kutoa amri hiyo basi imwamuru afuate matakwa ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kulinda haki za binadamu katika kutekeleza madaraka yake hayo.

68 Comments

  1. Hello, Neat post. There’s a problem together with your web site in web explorer, could test this… IE still is the marketplace leader and a large component to people will miss your excellent writing because of this problem.

  2. you are really a good webmaster. The site loading speed is incredible. It seems that you are doing any unique trick. Also, The contents are masterwork. you have done a great job on this topic!

  3. I used to be suggested this web site via my cousin. I’m now not positive whether this post is written by him as nobody else recognise such specific approximately my trouble. You are incredible! Thanks!

  4. I’m not that much of a internet reader to be honest but your blogs really nice, keep it up! I’ll go ahead and bookmark your site to come back later on. Many thanks

  5. My husband and i got very fortunate that Ervin managed to finish off his analysis with the precious recommendations he obtained when using the site. It’s not at all simplistic just to be giving out information which usually many people may have been selling. And now we see we have the website owner to appreciate for this. The main illustrations you have made, the easy site menu, the relationships you give support to foster – it is mostly amazing, and it’s really assisting our son in addition to the family feel that that theme is amusing, and that is extraordinarily pressing. Thank you for all!

  6. You could definitely see your enthusiasm within the work you write. The world hopes for more passionate writers such as you who are not afraid to mention how they believe. All the time go after your heart.

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*