Nukta ya Leo

MUHIMU KUJIFUNZA!!

  1. Kabla hujafanya jambo lolote jiulize?

Je, jambo hili linauwezo wa kunisogeza hata inchi moja kuelekea kwenye malengo yangu. Kama jambo hilo linauwezo huo basi ni vyema ukalifanyia kazi. Ila ukigundua haliwezi achana nalo.

 Dunia kwa sasa ina kelele nyingi sana ambazo usipokuwa makini zitakupoteza.

 Fanya yale mambo yanayokupeleka kwenye malengo yako. Lakini, kama huna malengo unaweza ukaafanya lolote na itakuwa sawa kwako.

  1. Jifunze kutumia muda wako mwingi kwa yale mambo yenye uwezo wa kubadili maisha yako.

Kama kuna jambo ambalo unaona unalifanya halina ‘impact’ kwenye maisha liache mara moja. Kwa mfano unapokuwa na kazi maalum acha kupoteza muda kwenye simu au kuchati.

  1. Usikate tamaa kwa sababu mambo yako yanakwenda hovyo. Usikate tamaa kwa sababu umeweka juhudi kwenye mambo yako na huoni matokeo chanya yakitokea.

 Endelea kuweka juhudi na kumbuka kabla mambo hayajawa mazurini kuna wakati huwa yanakuwa mabaya kwanza.

  1. Kanuni mojawapo kubwa ya kushindwa kwa kile unachokifanya, ni kufanya mambo kwa kawaida. Hakuna ambaye amewahi kufanikiwa sana kwa kufanya mambo kwa kawaida au kwa wastani.

Kama unafanya kazi kawaida kawaida katika maisha yako, hicho ni chanzo cha kushindwa katika mambo mengi. Kama unatafuta mafanikio makubwa, hakikisha usiwe mtu wa kawaida. Kila kitu unachotaka kufanya, kifanye kwa viwango vya hali ya juu sana. Hata inapotokea kuna vizuizi kuwe hakuna kitu ambacho kinaweza kukuzuia kufanikiwa kutokana na nguvu kubwa uliyoiweka.

  1. Mambo matatu ambayo watu maskini wanayafanya sana.

a/ Kukwepa majukumu.

b/ Kutoa sababu.

c/ Kulalamika.

“Average is falling formula”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*