Matumizi sahihi ya mabenki katika kukuza biashara

Kwa leo tuanze na maana pana ya neno financial institution ambamo mabenk pia yanaangukia hapo.

Zipo aina kuu mbili nazo ni taasisi za fedha zenye mamlaka ya kupokea amana (Deposits) toka kwa umma (na hapa ndipo mabenk kama CRDB,NMB,NBC,Akiba nk utazikuta)

na aina ya pili ni zile financial institutions ambazo kisheria hazijaruhusiwa kupokea amana toka kwa umma…mfano ni kama Sacco’s ,(Finca na pride ) zinaweza eleweka vyema hapo kwa sasa zipo in transition to commercial bank.)

 

Tuje katika maswala ya fursa na huduma ambazo unaweza kuzipata katika mabenki,

hizi ni pamoja na kuweka Akiba,kupata mikopo,kupata udhamin(Guarantee) mfano Tender guarantee,Letter of Credit {LC) na fursa nyingine nyingine.

Pia tusisahau juu ya ushauri (customer service) ambapo tinaweza pata consultations bure.. Mfano. Unahitaji kujua namna ya kuagiza mzigo kutoka ng’ambo. Ni namna gani unaweza kuwa salama wewe na pesa zako kwa asilimia 100%..pengine sasa hapa ndipo habari za guarantee utashauriwa na benki yako.

Mbali na kutunza pesa zetu…benki ni sehemu sahihi ambayo kwa visionary person anatakiwa kuwa karibu nayo…kwani ni sehem nyeti sana kama ilivyo kwa vijiwe ambapo taarifa za mwenendo wa uchumi hupatikana kwa haraka..mfano utajua habari za hisa, ukuwaji au ushukaji wa thamani wa pesa za kigeni n.k

Pia hapo ndipo unaweza kupata ushauri wa bure juu ya kukuza biashara yako kupitia mikopo ambayo ni linganifu na ukifuata makubaliano HAKIKA huwezi kufeli…aina za mikopo ni mingi kulingana na mahitaji au nature ya biashara yako.

Baadhi ya aina za mikopo ni pamoja na mikopo wa binafsi kwa walioajiriwa…salaried loan.. Huu ni mkopo rahic na hakuna presha kwani malipo yake hutoka ktk mshahara..ni mikopo kwenye riba ndogo kwa mabenki yote ukilinganisha na mikopo mingine na mashart ya upatikanaji ni rahisi…

.mikopo mingine ni ya kufanyia kazi(working ) mfano kuongeza uwezo wa kununua bidhaa,kuagiza bidhaa..nk. Mikopo hii pia ya kufanyia kazi imegawanyika katika makundi mawili makubwa nayo ni Overdraft..na instalment loan..zote zitafafanuliwa baadae zaid

Vigezo vya kupata fursa za mikopo kwa uchache ni pamoja na:-

1.Wazo zuri….andiko

2.Uchambuzi wa upungufu wa mtaji unaojitosheleza..

3.Kadilio la mtiririko wa fedha,,cash flow projection ambayo ni realistic

4.Usimamizi usiotia shaka

5.Dhamana ya mikopo hitajika…hiz ni baadhi tu zikiambatana na

 

a)Business legalities eg.TIN,Business licence na TRA tax clearance

b)Uzoefu wa kufanya biashara na mazingira utakayofanyia

c)Mzuunguuko wa akaunti yako (account turnover..mfano mabenki yangependa kuona unachoweza kukopa ni 25% ya jumla ya mzunguuko wako..(Note.Account turnover)

 

Jambo  jingine la kujua ni katk mabenki tu riba za mikopo ni ndogo na ni kati ya 18%-36 kwa mwaka. Wakati taasisi tofauti na mabenki hutoza kati ya 8%-15% kwa mwezi na hivyo kufanya mkopaji alipe kati ya 96%-180% kwa mwaka

Benki inapata amana ambazo huzilipia riba ndogo ukilinganisha na riba inayokopeshea…mfano..inaweza toa riba ya asilimia 4 kwa mwaka ilihali itakopesha kwa 20%.

Pili inaweza kuwekeza katika hati fungani (Treasury Bills -hazina juu ya Nchi) ambako huweza kuvuna pesa nyingine zaid

(by Mr Danford Muyango-Meneja biashara CRDB- UDOM)

 

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*