Azam yazipiga bao Simba, Yanga

KLABU ya Azam imevipiga bao vigogo vya Simba na Yanga baada ya kuwa ya kwanza kumsajili wachezaji kutoka nje katika dirisha dogo la usajili.

Azam FC jana iliingia mkataba na wachezaji wawili wa Ghana, Samuel Afful na Mohamed Abdul walioingia mikataba ya miaka mitatu na miwili.

Afful mwenye umri wa miaka 21 ni mchezaji wa kulipwa kutoka klabu ya Sekondi Hasaacas inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo wakati Abdul alikuwa akikipiga katika timu ya Aduana Stars.

Afful ni mshambuliaji mwenye uzoefu wa hali ya juu amezichezea kwa nyakati tofauti amezichezea timu kibao za Ghana zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Novemba mwaka 2013, kocha Maxwell Konadu, alimuita Afful katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana ya Black Stars, ambacho kilishiriki mashindano ya kimataifa ya Afrika Magharibi yanayoshirikisha wachezaji wa ndani. Mchezaji huyo aliisaidia Ghana kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuisaidia timu hiyo kuifgunga Senegal kwa mabao 3-1.

Mbali na Ghana na Senegal mataifa mengine yaliyoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Liberia, Niger na Sierra Leone.

Sekondi Hasaacas FC ilipanda daraja na kucheza Ligi Kuu ya Ghana mwaka 2013 na maskani ya timu hiyo yako Sekondi-Takoradi.

Abdul ndiye mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Ghana, ambapo amefunga mabao 15 hadi sasa.

Kocha wa Azam FC, Zeben Hernandez alisema kuwa amefurahi kwa wachezaji hao kusajiliwa na timu yake kwani ana imani wataisaidia sana katika mashindano ya nyumbani na kimataifa.

66 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*