Mbunge Lema ashindwa kufikishwa mahakamani

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana alishindwa kufikishwa mahakamani kwa sababu zisizojulikana kusikiliza maelezo ya awali katika kesi inayomkabili yeye na mkewe, Neema Lema (33) jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ambako wanatuhumiwa kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Kukosekana kwa mbunge huyo mahakamani, kulimlazimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augustino Rwezile kutoa amri ya kutolewa hati ya kumtoa mahabusu mshitakiwa huyo na kumleta mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe maelezo ya awali.

Hata hivyo, tangu amri hiyo itolewe saa nne asubuhi hadi saa saba mchana jana, mshitakiwa hakufikishwa mahakamani hapo licha ya mke wake kuwepo hapo. Rwezile alimtaka Wakili wa Serikali, Fortunatus Mhalila kueleza sababu za kushindwa kumleta Lema mahakamani wakati mahakama imetoa amri.

Mhalila alidai mshitakiwa ameshindwa kufikishwa mahakamani kutokana na sababu zisizojulikana, ila kwa sababu upelelezi umekamilika, aliomba mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za awali. Majibu hayo yalipingwa na Wakili wa utetezi, John Mallya aliyetaka kufahamu sababu za kutofikishwa anazodai hazikuweza kuzuilika ni zipi na vema zikatajwa mahakamani.

“Mheshimiwa hakimu hizo sababu zisizoweza kuzuilika ni zipi Wakili wa Serikali atueleze, tujue kama sio amedharau mahakama licha ya kutakiwa kumleta mshitakiwa,” alieleza Mallya na kumfanya Hakimu Mfawidhi Rwezile kusisitiza hati ya kumtoa mahabusu itolewe ili aletwe mahakamani leo katika kesi hiyo ambayo itasikilizwa hoja za awali.

Awali katika kesi hiyo, Lema na mkewe Neema, alisomewa mashitaka kuwa kati ya Agosti 20, mwaka huu ndani ya Arusha, walimtumia ujumbe kupitia simu ya kiganjani mkuu huyo wa mkoa wenye lugha ya matusi huku wakijua ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulituma kutoka 0764150747 namba 0756551918 kwenda namba 0766- 757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni wanavyothibiti mashoga.”

Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipatiwa dhamana hadi litakaposomwa leo.

Katika hatua nyingine, waandishi wa habari walijikuta kwenye wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kutokana na askari wa Jeshi la Polisi na wenzao wa Magereza kuwazuia kuingia chumba cha mahakama na kuwafukuza nje ya uzio wa mahakama kwa madai kuwa ni maagizo ya mahakama.

71 Comments

  1. “I have mastered some new points from your web site about personal computers. Another thing I have always assumed is that computer systems have become something that each household must have for a lot of reasons. They supply you with convenient ways in which to organize households, pay bills, go shopping, study, hear music and in many cases watch shows. An innovative method to complete most of these tasks is with a notebook computer. These desktops are mobile, small, strong and easily transportable.”

  2. “Nice post. I learn something totally new and challenging on sites I stumbleupon every day. It’s always exciting to read through articles from other writers and practice something from their sites.”

  3. Its like you read my mind! You appear to know so much about this, like you wrote the book in it or something. I think that you could do with some pics to drive the message home a bit, but instead of that, this is fantastic blog. A fantastic read. I’ll certainly be back.

  4. Very good website you have here but I was curious if you knew of any discussion boards that cover the same topics discussed here? I’d really like to be a part of group where I can get advice from other knowledgeable people that share the same interest. If you have any recommendations, please let me know. Thanks a lot!

  5. Hey There. I found your blog the use of msn. This is a very neatly written article. I’ll make sure to bookmark it and come back to read more of your useful info. Thank you for the post. I’ll definitely return.

  6. “We are a group of volunteers and starting a new scheme in our community. Your web site provided us with valuable info to work on. You have done an impressive job and our whole community will be grateful to you.”

  7. Fantastic beat ! I would like to apprentice while you amend your website, how can i subscribe for a blog website? The account helped me a appropriate deal. I were a little bit acquainted of this your broadcast provided vivid clear concept

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*