Msajili vyama vya siasa avifutia usajili vyama vitatu

Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi amevifutia usajili vyama vitatu ambavyo ni chama cha Ustawi wa Jamii CHAUSTA, APPT maendeleo na JAHAZI ASILIA.

Jaji Mutungi amefikia uamuzi huo kutokana kuwa vyama hivyo vimekuwa na ofisi upande mmoja jambo ambalo ni kinyume na kifungu 10d ambacho kinakitaka chama cha siasa kuwa na ofisi pande mbili kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Lakini sasabu ya pili ni kutokuwa na wanachama Zanzibar kwa mujibu wa kifungu 10b pia kushindwa kuweka wazi mapato na matumzi ya fedha za chama kama kifungu cha 14 (1) (a) kinavyoelekeza.

(Chanzo-Mtanzania)

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*