Pluijm aikubali Mbeya City

KOCHA wa Yanga, Hans van Pluijm ameikubali Mbeya City na kusema ni timu nzuri yenye uwezo wa kucheza dakika 90 kwa ushindani.

Aidha kocha huyo amelaumu wachezaji wake kutokuwa makini mwanzoni mwa mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City kwa kuruhusu kufungwa bao la mapema.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, Yanga ililala kwa mabao 2-1. Pamoja na malalamiko hayo kwa wachezaji wake, Pluijm amemlaumu mwamuzi Rajab Mrope wa Ruvuma kuwa ndio amewanyonga katika mchezo huo.

Pluijm alisema kuwa bao la pili katika mchezo huo halikustahili kwani maamuzi yake yalikuwa na utata na kwamba aliwaamuru wachezaji wake warudi nyuma kabla ya filimbi kupigwa na Mbeya City wakatumia mwanya huo kufunga.

“Mbeya City ni timu nzuri, wana uwezo wa kucheza dakika 90 bila kuchoka na timu ndio inavyotakiwa kuwa, lakini mwamuzi hakuwa makini, amewaumiza wachezaji wangu kiakili na kuwatoa mchezoni, aliwasababisha wacheze chini ya kiwango,” alisema Pluijm ambaye amedai kuwa anajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Prisons.

“Naweza kusema ilikuwa ni siku mbaya kwetu, wachezaji wangu wameniangusha hawakucheza soka ninalolihitaji, hata hivyo, natumaini mchezo ujao tutacheza vizuri,” alisema.

Kwa matokeo hayo, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanabaki na pointi zao 27 wakiwa wamecheza mechi 13 wakiwa nyuma ya pointi nane dhidi ya mahasimu wao Simba ambao wana pointi 35 wakicheza michezo 13 sawa na Yanga.

Katika hatua nyingine Mwandishi Rahel Pallangyo anaripoti kuwa Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri amefurahishwa na ushindi huo licha ya kumlaumu mshambuliaji Ditram Nchimbi kwa kukosa bao la wazi. Nchimbi alishindwa kutumia nafasi ya wazi aliyoipata akiwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ kwani alipiga mpira uliopita nje kidogo ya goli.

“Tungeshinda bao tatu au pengine na zaidi ila Nchimbi kaninyima bao langu la wazi kabisa, pale alitakiwa kumzunguka kipa na kufunga ila sijui aliwaza nini, kikubwa nimefurahi kuifunga Yanga,” alisema Phiri.

Pia Phiri alisema mechi ilikuwa na presha tangu maandalizi yake hata wachezaji wa Yanga kipindi cha pili walianza kucheza rafu lakini amefurahi kupata pointi tatu na kudai anakwenda kumalizia ushindi kwa Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki hii.

Phiri alisema aliwaeleza wachezaji watafute ushindi wa haraka maana aliwaona Yanga mechi za nyuma kuwa wakicheza dakika kadhaa wanapoteza nguvu na baada ya kupata matokeo aliwataka wacheze kwa kuzuia ili washambuliaji wao wasipate nafasi ya kupita.

Imeandikwa na Vicky Kimaro-Habari Leo

87 Comments

  1. “Hello There. I found your blog using msn. This is an extremely well written article. I will make sure to bookmark it and return to read more of your useful info. Thanks for the post. I will definitely return.”

  2. Zune and iPod: Utmost These look at the Zune to the Contact, still once seeing how slim and amazingly minor and gentle it is, I think about it in the direction of be a rather exclusive hybrid that brings together features of equally the Touch and the Nano. It truly is amazingly colorful and gorgeous OLED show is somewhat smaller than the contact screen, still the player itself feels Really a bit scaled-down and lighter. It weighs relating to 2/3 as significantly, and is considerably smaller sized inside width and peak, despite the fact that getting specifically a hair thicker.

  3. Sick and tired of being bored? There’s nothing at all good to watch on TV these days. How many cat videos can you watch at YouTube? What you really want is some live adult entertainment. That’s what http://www.camgirl.pw is all about. It’s 24/7 excitement like you’ve never seen before. Check it out and tell a friend. Something this good needs to be shared.

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*