Wabunge wahitaji tathimini mpango maendeleo ya taifa

WABUNGE wameitaka Serikali kuleta bungeni tathimini ya utekelezaji wa robo mwaka wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2016/2017 kujiridhisha namna ulivyofanyiwa kazi kabla ya kupitisha mpango mpya wa mwaka huu.

Aidha, wametaka mpango wa maendeleo uweke nguvu katika mambo yanayogusa wananchi moja kwa moja, ikiwemo maji, afya (dawa), elimu na ajira na kutaka miradi mikongwe nchini; wa makaa ya mawe Mchuchuma na wa chuma wa Liganga, unatekelezwa kuongeza ajira kwa wananchi.

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya Serikali wa mwaka huo, yaliwasilishwa jana bungeni mjini hapa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

Katika mapendekezo hayo yaliyowasilishwa juzi, Serikali imepanga kutumia Sh trilioni 32.946 katika bajeti yake ya Mwaka wa Fedha 2017/18.

Mwaka 2016/17 mpango unaotekelezwa sasa ukiwa katika robo ya pili ya mwaka, ilikuwa Sh trilioni 29.5. Akichangia mjadala wa mapendekezo hayo wakati Bunge lilipokaa kama kamati jana, Mbunge wa Mbinga, Sixtus Mapunda, aliipongeza Serikali kwa mpango mzuri, lakini alisema ni lazima kurejea mafanikio na changamoto za mpango uliopita ili kujitathimini na kujua nini kishauriwe kwa mpango mpya.

Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni (CCM), alimtaka Dk Mpango kusikiliza ushauri wa wabunge na kulieleza bunge mpango wa mwaka jana (unaotekelezwa sasa) umeleta mabadiliko gani ili washauri nini kifanyike kwa mpango ujao.

Suala la tathimini pia lilijadiliwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) aliitupia lawama Serikali kuwa haijaleta bungeni taarifa ya mpango uliopita na kuhoji Serikali imejipangaje kupeleka fedha katika halmashauri kwa kuwa miradi inakwama.

(Chanzo-Habari Leo)

81 Comments

  1. I precisely wished to thank you very much once again. I do not know the things that I would’ve taken care of in the absence of these basics contributed by you concerning this subject. Entirely was an absolute traumatic setting in my circumstances, but coming across the very well-written tactic you handled it forced me to jump over happiness. Extremely happier for this assistance and then sincerely hope you find out what a great job that you are providing teaching the mediocre ones using your website. Most likely you have never met any of us.

  2. Wow that was unusual. I just wrote an incredibly long comment but after I clicked submit my comment didn’t show up. Grrrr… well I’m not writing all that over again. Anyhow, just wanted to say excellent blog!

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*