Viongozi Chadema kortini Tabora

JESHI la polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora limewakamata na kuwafikisha mahakamani viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Waliofikishwa katika mahakamani ya hakimu mkazi ni Katibu wa chama hicho wilaya ya Igunga, Idd Ndagwemeleye (54) mkazi wa mtaa wa Mwayunge, Aluhanya Ngozo (48) mkazi wa kitongoji cha Mwamsunga ambaye ni katibu wa tawi katika kitongoji hicho na Fea Lipa (41) mkazi wa Mwamsunga ambaye ni Mwenyekiti wa tawi la Mwamsunga.

Aidha, mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama jana mbele ya hakimu wa wilaya, Ajali Millanzi kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo, Oktoba 30, mwaka huu, kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni katika kitongoji cha Mwamsunga.

Alidai washtakiwa wote kwa pamoja wakiwa wafuasi na viongozi wa Chadema walifanya mkusanyiko usiokuwa halali ambao ungeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Aidha, alisema washitakiwa wote hao wanatuhumiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu 74 na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, washitakiwa wote walikana kutenda makosa hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 10, mwaka huu, itakapotajwa tena na washitakiwa wote wako nje kwa dhamana ya Sh 700,000 kila mmoja.

Mahakama hiyo imepiga marufuku kwa muda usiojulikana kwa viongozi hao kufanya mikutano isiyoruhusiwa kisheria hadi kesi yao iliyopo mahakamani itakapokwisha.

(Chanzo-Habari Leo)

52 Comments

  1. “I have seen plenty of useful elements on your internet site about desktops. However, I have got the impression that laptop computers are still less than powerful more than enough to be a good option if you frequently do things that require a lot of power, for example video enhancing. But for net surfing, word processing, and the majority of other frequent computer work they are okay, provided you may not mind the tiny screen size. Thanks for sharing your ideas.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*