Taasisi ya Ulinzi, Usalama na Siasa ya SADC yakutana Dar leo

Taasisi ya Ulinzi, Usalama na Siasa ya SADC imekutana Jijini Dar es Salaam leo kujadili masuala mbalimbali likiwemo swala la Uchaguzi Mkuu nchini Congo DRC.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kabla yakuanza mukutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustino Mahiga, alisema kuwa tangu Rais Dk. John Magufuli ashike nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo, amekuta matatizo mengi yanayohitaji kutatuliwa.

Amesema miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni hali ya siasa nchini Lesotho ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

(Chanzo-Mtanzania)

75 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*