Obama: Mustakabali wa dunia utakuwa kwenye mizani

Rais wa Marekani Barack Obama ametahadharisha kwamba wapiga kura nchini Marekani watakuwa wakiamua kuhusu hatima ya Marekani kama taifa na ulimwengu kwa jumla watakapokuwa wanapiga kura Jumanne.

Ametoa wito kwa wafuasi wa chama cha Democratic wa asili zote kujitokeza kwa wingi na kumpigia kura Bi Hillary Clinton.

Amesema mpinzani wa Bi Clinton, Donald Trump wa chama cha Republican ni tishio kwa haki za kiraia ambazo watu wamezipigania kwa miaka mingi.

Rais Obama alikuwa anahutubu katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Carolina Kaskazini.

Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?

biliclinton

Swali ambalo limekuwa likiulizwa tangu kubainika kwa uwezekano kwamba Bi Hillary Clinton anaweza akawa rais wa Marekani ni jina ambalo mumewe atapewa.

Kwa sasa Bi Clinton, anayewania urais kupitia chama cha Democratic, amekuwa akiongoza katika kura za maoni kitaifa na katika majimbo mengi yanayoshindaniwa.

Wengi wamekuwa wakichakura kwenye Google.

Katika ngazi ya kimataifa, nafasi kama atakayoichukua Bw Bill Clinton si jambo geni. Mumewe Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Joachim Sauer, ambaye ni mprofesa wa kemia, huitwa jina lake tu.

Mfadhili Philip John May, mumewe waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, sawa na Ujerumani, hana jina rasmi.

Lakini nchini Marekani, kumekuwa na utamaduni wa kumrejelea Rais na Mke wa Rais ambaye huitwa First Lady na ambaye kwa Kiswahili huitwa Mama wa Taifa.

Hillary Clinton atabahatika mara ya pili?

clintonh

Hillary Clinton amehudumu katika nyadhifa nyingi siasa za Marekani, alikuwa mama wa taifa, seneta, waziri wa mambo ya nje. Sasa, anajaribu kwa mara ya pili kutimiza ndoto yake kuu, kuwa rais wa Marekani

Mwanasiasa huyu wa Democtratic wa umri wa miaka 68 alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Rais Barack Obama mwanzoni mwa utawala wake Januari 2009.

Alijiuzulu muda mfupi baada ya Rais Obama kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.

Ni mwanadiplomasia mashuhuri Marekani na anafahamika sana kwa kusafiri sana nchi mbalimbali na kufuata diplomasia ya kukutana ana kwa ana na wahusika.

Kuzoea kwake kufanya safari nyingi za kuchosha, kunamuandaa vyema kwa changamoto za safari nyingi za kampeni za urais.

Alijaribu mara ya kwanza kuwania urais lakini akashindwa na Rais Obama wakati wa mchujo wa chama cha Democratic mwaka 2008.

Hillary Rodham Clinton

 • Alizaliwa 26 Oktoba, 1947 mjini Chicago
 • Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Sheria cha Yale, 1973
 • Aliolewa na Bill Clinton mwaka 1975
 • 1993-2001: Alipigania kupanuliwa kwa bima ya afya na haki za wanawake alipokuwa mama wa taifa
 • Alichaguliwa seneta wa New York mwaka 2000
 • Alichaguliwa tena kwa kura nyingi 2006
 • 2008: Alishindwa mchujo wa kuteua mgombea urais chama cha Democratic
 • 2009-2013: Alihudumu kama Waziri wa mambo ya nje

Hillary Diane Rodham alizaliwa Oktoba 1947 mjini Chicago. Miaka ya 1960 alihudhuria masomo Chuo cha Wellesley jimbo la Massachusetts, na akaanza kujihusisha na siasa za wanafunzi.

Alisomea uanasheria katika Chuo Kikuu cha Yale ambapo alikutana na Bill Clinton. Walifunga ndoa 1975. Aliendelea kujihusisha na siasa baada ya Bw Clinton kuwa gavana wa Arkansas mwaka 1978.

Bw Clinton alipokuwa akifanya kampeni za urais mwaka 1992, alisema kwa mzaha kwamba alikuwa anawapa wapiga kura marais wawili “kwa bei ya mmoja”.

Lakini Bw Trump amesema Bw Obama anafaa kuacha kumfanyia kampeni Bi Clinton na badala yake aangazie kuongoza nchi.

“Ukweli ni kwamba, hakuna anayetaka miaka mingine minne ya Obama,” ameambia wafuasi Pensacola, Florida.

Amesema sifa halisi za Bi Clinton zimedhihiriska siku za karibuni.

“Hatima ya jamhuri yetu imo kwenye mabega yengu,” Rais Obama ameambia wafuasi wa chama cha Democratic katika jimbo linaloshindaniwa la Carolina Kaskazini.

“Hatima ya dunia imo hatarini nanyi pia, Carolina Kaskazini, tutahakikisha kwamba tunaielekeza katika njia ifaayo.

hilari

“Simo kwenye karatasi za kura, lakini nawaambia – usawa umo kwenye karatasi za kura, maadili yanapigiwa kura, haki imo kwenye kura, ufanisi umo kwenye karatasi za kura; demokrasia yetu imo kwenye kura.”

Kampeni ya Bi Clinton imetikiswa na tangazo la mkuu wa FBI James Comey kwamba kuna barua pepe mpya kuhusu mgombea huyo zinazochunguzwa.

Bw Comey ameshutumiwa vikali kwa kutangaza habari hizo siku 11 kabla ya tarehe ya uchaguzi.

Awali, Bw Obama alimkosoa hadharani kwa kuanzisha tena uchunguzi na kusema katika utamaduni wa Marekani, hatua huwa hazichukuliwi kwa kutegemea “maelezo ambayo hayajakamilika.”comey

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Bw Obama kuzungumza hadharani tangu Bw Comey atangaze Ijumaa kwamba FBI wamepata barua pepe mpya ambazo huenda ziwe zinahusiana au huenda zisiwe zinahusiana na uchunguzi wa awali ambao ulikuwa umefanywa dhidi ya Bi Clinton.

Bi Clinton alikuwa ametuhumiwa kutumia sava ya barua pepe ya kibinafsi kufanya shughuli rasmi za serikali jambo ambalo baadhi wanasema lilihatarisha usalama wa taifa.


Barua pepe hizo mpya zilipatikana kwenye uchunguzi dhidi ya mbunge wa zamani Anthony Weiner anayetuhumiwa kumtumia msichana wa miaka 15 ujumbe wa kimapenzi jimbo la Carolina Kaskazini.

Bw Weiner ni mumewe mmoja wa wasaidizi wakuu wa Bi Clinton, Huma Abedin.

(Chanzo-BBC)

 

99 Comments

 1. “you’re actually a good webmaster. The site loading speed is incredible. It kind of feels that you are doing any distinctive trick. Also, The contents are masterpiece. you’ve done a fantastic job in this matter!”

 2. “Awesome blog you have here but I was wondering if you knew of any forums that cover the same topics talked about here? I’d really like to be a part of group where I can get suggestions from other experienced people that share the same interest. If you have any recommendations, please let me know. Bless you!”

 3. “Hey there! I know this is somewhat off topic but I was wondering which blog platform are you using for this website? I’m getting fed up of WordPress because I’ve had issues with hackers and I’m looking at options for another platform. I would be great if you could point me in the direction of a good platform.”

 4. I would not even know generate income ended up in this article, on the other hand presumed that submit once were beneficial. I can’t have an understanding of that you happen to be having said that surely you’ll a new famous tumblr when you are definitely not previously koleksi youtube terbaru. Many thanks!

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*