Mashitaka mauaji watafiti yabadilishwa

WASHiTAKIWA 13 wa mauaji ya watafiti watatu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian (SARI) jijini Arusha, wamesomewa upya mashitaka mapya jana.

Kila mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka matatu ya mauaji. Awali, walisomewa shitaka moja la kuwaua watu watatu kwa wakati mmoja.

Washitakiwa hao ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Iringa Mvumi, Albert Chimanga (58), Cecilia Chimanga (34), Sostheness Mseche (35) ambaye ni Mwinjilisti, Julius Chimanga (35), David Chimanga (44), Dorca Mbehu (55), Edna Nuno (47), Grace Msaulwa (41), Juma Madehe (44), Lazaro Kwanga (35), Yoram Samamba (55), Edward Lungwa (39) na Simon Samamba (22).

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini, Joseph Fovo, washitakiwa walisomewa mashitaka na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Beatrice Nsana ambaye katika shitaka la kwanza, ilidaiwa Oktoba mosi mwaka huu, katika kijiji cha Iringa Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, washtakiwa kwa pamoja walimuua Nicas Magazine.

Katika shitaka la pili, washtakiwa hao wanadaiwa kumuua Faraja Mafuru na katika shtaka la tatu, washtakiwa hao wanadaiwa kumuua Theresia Nguma. Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Walipelekwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Novemba 14, mwaka huu.

Mauaji hayo yalitokea Oktoba mosi mwaka huu. Watafiti wawili na dereva wao waliuawa na kisha miili yao kuchomwa moto baada ya kuhisiwa kuwa ni wanyonya damu.

Walifika kwenye eneo hilo wakiwa na gari lenye namba za usajili STJ 9570 aina ya Toyota Hilux Double, mali ya Kituo cha Utafiti cha SARI Arusha.

Awali ilidaiwa watu hao walivamiwa na wanakijiji wa Iringa Mvumi na kuwakata kwa mapanga na silaha za jadi kisha kuwachoma moto hadi kufa.

Chanzo cha tukio hilo ni Cecilia Chimanga kupiga yowe kuwafahamisha kwamba ameona watu anaohisi ni wanyonya damu (mumiani).

(Chanz0-Habari Leo)

86 Comments

  1. “I’m not sure where you’re getting your info, but good topic. I needs to spend some time learning much more or understanding more. Thanks for fantastic info I was looking for this info for my mission.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*