Wadaiwa kughushi nyaraka kutapeli mamilioni

WAFANYABIASHARA wawili maarufu jijini Arusha, Ralph Kyarua (40) na Fredrick Lyaruu (42), wamepandishwa kizimbani kujibu mashitaka la kutapeli na kughushi nyaraka  za bima na kujipatia mamilioni fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wafanyabiashara hao ambao ni Wakurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Millennium iliyopo eneo la Mnara wa Saa, Barabara ya Boma jijini hapa, wanadaiwa kufanya utapeli huo kwa kuuza nyaraka bandia kwa nyakati tofauti jijini hapa na Moshi na kuingizia serikali hasara ya mamilioni.

Washitakiwa hao walisomewa mashitaka matatu na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Augustino Kombe mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Arumeru, Bernard Mganga, ilielezwa kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Januari na Desemba 17, mwaka jana eneo la Mnara wa Saa Arusha na kujipatia mamilioni ya fedha.

Kombe alidai shitaka la kwanza ni kufanya biashara bila ya leseni ya serikali, la pili ni kughushi nyaraka za magari na leseni za magari na kujipatia mamilioni ya fedha na shitaka la tatu ni kimiliki nyaraka za bima na stika zake za kughushi na kuibia serikali mamilioni ya fedha.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, waliyakana na wako nje kwa dhamana ya watu wawili kila mmoja na washitakiwa hao wanatetewa na wakili Robert Rogart anayemiliki Kampuni ya Ideal ya jijini hapa.

Wadhamini walipaswa kuwasilisha hati ya dhamana ya Sh milioni 20 kila mdhamini, washitakiwa walipaswa kukabidhi hati za kusafiria na hawaruhusiwi kutoka nje ya mkoa bila ya kibali cha mahakama. Pia wanatakiwa mara moja kwa mwezi kuripoti Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Arusha.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 28, mwaka huu kwani upelelezi haujakamilika.

(Chanzo-Habri Leo)

11 Comments

  1. “I’m not certain the place you are getting your information, however great topic. I must spend a while learning more or working out more. Thank you for magnificent info I was searching for this info for my mission.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*