CCM: Wanaomkosoa JPM ni waathirika wa mfumo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema wanasiasa wanaolalamikia na kushutumu uongozi wa Rais John Magufuli katika kipindi chake cha mwaka mmoja aliokaa madarakani ni wale walioathirika na mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na kiuchumi alioufanya.

Aidha kimemtaka Waziri Mkuu wa zamani ambaye alikuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa kutafakari dhana pana ya demokrasia iliyopo nchini kabla ya kumshutumu Rais Magufuli kwamba anakiuka misingi yake.

Katika hatua nyingine, chama hicho kikongwe nchini, kimevialika vyombo vya dola kufanya uchunguzi dhidi ya wenyeviti wa zamani wa kamati za kudumu za Bunge waliokuwa wakisimamia mashirika ya umma ambayo sasa yamebainika kufanya vibaya katika utendaji kazi wake.

Msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kauli ya hivi karibuni ya Lowassa kuwa ndani ya mwaka mmoja wa Rais Magufuli, demokrasia imeminywa na utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.

Ole Sendeka alisema CCM inashangazwa na hatua ya Lowassa kumpinga Rais kwa kuwadhibiti watumishi wa umma wanaokiuka maadili na kurudisha nidhamu, kuwadhibiti wala rushwa, kwa kuzilinganisha juhudi hizo na kaa la moto.

Alisema kiuhalisia wanaoona utumishi wa umma ni kaa la moto ni wale wasiokubali kufuata kanuni na taratibu za utumishi wa umma na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itazidi kusonga mbele katika kuweka nidhamu serikalini.

Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuanza kuhimiza demokrasia ndani ya vyama vyao kabla ya kuzungumzia demokrasia iliyopo ndani ya CCM.

Kuhusu wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge ambao walikuwa wakisimamia mashirika ambayo sasa yanatajwa kufanya vibaya ikiwemo Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF, Ole Sendeka alisema ni vema wenyeviti hao wakachunguzwa ili kubaini kiasi cha fedha walizonazo, huku akimtaja aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Mjini – ACT Wazalendo) kuwa miongoni mwao.

67 Comments

  1. “One more important issue is that if you are a senior citizen, travel insurance pertaining to pensioners is something you need to really think about. The mature you are, the greater at risk you might be for getting something negative happen to you while in foreign countries. If you are not covered by many comprehensive insurance, you could have many serious issues. Thanks for sharing your hints on this web site.”

  2. “I’m curious to find out what blog platform you happen to be using? I’m having some minor security issues with my latest blog and I would like to find something more safe. Do you have any suggestions?”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*