Hifadhi kubwa kujengwa bahari ya Antaktika

_92120387_cf8bc89b-998a-420b-b117-47ea20b9d11e

Miaka ya mazungumzo ya kimataifa imefikia kilele chake kwa makubaliano ya kujenga hifadhi kubwa ndani ya bahari katika maji safi ya Antaktika.

Nchi ya New zealand na Marekani zimepewa jukumu la kusimamia 1.57 milioni kilomita za mraba za eneo la bahari zinazolindwa katika bahari ya Ross, ambayo ni makazi ya mamilioni ya penguins.

Japo Urusi inazuia mpango huo lakini waziri wa mambo ya nje wa New zealand Murray McCully, amesema kuwa mataifa ishirini na nne yaliyoshiriki mazungumzo hayo yamefikia makubaliano ya kusawazisha ulinzi wa bahari na kuendesha uvuvi na tafiti endelevu za kisayansi.

49 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*