Maafisa: Al-Shabaab sio waliotekeleza shambulio la Mandera

_92077405_ff38ee87-30bd-43a3-be44-c44f574d2910

Shambulio la usiku katika mji wa Mandera nchini Kenya limetekelezwa na wanamgambo wasio al-Shabab, kwa mujibu wa mratibu wa usalama wa eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya Bw Mohamud Saleh.

Mandera inapakana na Ethiopia na Somalia.

Kundi la Al-Shabab Somalia tayari limekiri kuhusikana shambulio hilo dhidi ya nyumba ya malazi , kama tulivyoarifu awali.

Lakini Bwana Saleh amesema kutokana kuwa mpka na Somalia hufungwa kuanzia usiku hadi alfajiri , hakuna namna kwa washambuliaji kuvuka mpaka huo.

Ameongeza kuwa uchunguz wa awali umedhihirisha kuwa shambulio hilo la saa tisa alfajiri lilitekelezwa na “magengi ya wahalifu walio na itikadi kali waliopo katika mji wa Mandera ambao wametumia vilipuzi vinne kuilipia nyumba hiyo ya malazi”.

Watu 12 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba hiyo ya malazi mjini Mandera.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe amesema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Bishaaro.

Wanamgambo walirusha vilipuzi kwenye nyumba hiyo kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi waliokuwemo ndani.

“Sehemu ya jumba iliporomoka, na kuua watu 12. Watu sita wametolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo wakiwa hai kufikia sasa,” ameandika Bw Kiraithe kupitia mtandao wa Twitter.

Wataalamu wa mabomu wanafanya uchunguzi kubaini ni vilipuzi vya aina gani vilitumiwa kutekeleza shambulio hilo.

_92076693_swahilimanderakenyalocator

Awali kundi la al-Shabaab limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali._92077407_20ace0f6-60b4-46c0-a575-7e955a074c6e

8 Comments

  1. “I’ve been absent for a while, but now I remember why I used to love this web site. Thanks , I’ll try and check back more frequently. How frequently you update your site?”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*