CCM wamdhibiti Maalim Seif Zanzibar

-

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibada kwa shughuli za kisiasa visiwani humo.
Tamko hilo limetolewa siku moja baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kutoa siku saba kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kuchukua hatua dhidi ya wanasiasa wanaohubiri siasa kwenye nyumba za ibada.
Umoja huo ulisema kama SMZ itashindwa kuchukua hatua, wataingia mitaani kuuthibitishia ulimwengu kuwa hakuna utii wa sheria visiwani humo wakimtuhumu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kujihusisha na vitendo hivyo.
Akitoa tamko la Serikali Zanzibar jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema Serikali inawaagiza Wakuu wa mikoa yote Zanzibar kusimamia utekelezaji wa agizo hilo katika mikoa yao.
“Kwa taarifa hii, Serikali inawaagiza Wakuu wa mikoa kupitia Kamati zao za Ulinzi na Usalama, kusimamia utekelezwaji wa agizo hili katika mikoa yao,” alisema Mohammed.
Alisema Serikali imewaagiza Wakuu wa mikoa kuwachukulia hatua za kisheria mtu yeyote ambaye atakiuka agizo hilo.
Aliongeza kuwa, viongozi wa dini na Kamati zao katika nyumba za ibada ambao watawaruhusu wanasiasa kufanya shughuli za kisiasa watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mohammed alisema hivi karibuni katika baadhi ya maeneo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika Misikiti ya Mbuyuni, Kihibnani na Kwabiziredi, kumetokea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kupita na kutoa hotuba za kisiasa katika Misikiti hiyo.
“Shughuli za vyama vya siasa zinaendeshwa na sheria namba 5 ya mwaka 1992 inayoelewa wazi mipaka na shughuli za kisiasa ziendeshwe chini ya sheria hiyo.
“Vitendo vinavyofanywa na viongozi wa kisiasa wanaotumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa ni kinyume na dhamira ya Katiba na Sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya Mwaka 1992,” alisisitiza.
Alisema shughuli zote za dini ya Kiislamu Zanzibar zinasimamiwa kupitia Sheria Namba 9 ya Mwaka 2001, Namba 2 ya Mwaka 2007 na Namba 3 ya Mwaka 1985 zinazoongoza Taasisi mahsusi kama Ofisi ya Mufti, Mahakama ya Kadhi na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.
Aliongeza kuwa, kupitia katiba na sheria, uhuru wa mtu kuabudu dini anayoitaka umetolewa bila kuingiliwa na itikadi za vyama vya siasa kama inavyobainishwa na katiba zote mbili ibara ya 19 ambazo zinaeleza umuhimu wa uhuru wa mtu kuamini dini aitakayo kwa misingi ya kukuza usalama na amani katika jamii.
Mohammed aliwataka wananchi kuzitumia nyumba za ibada kwa shughuli za kidini kama ilivyokusudiwa, kuacha kushirikiana na viongozi au wananchi wengine wanaotumia nyumba za ibada kujinufaisha kwa maslahi binafsi ya kisiasa.
H i v i k a r i b u n i , UVCCM walimtuhumu Maalim Seif akidaiwa kupita katika baadhi ya Misikiti siku ya Ijumaa, kutoa matamshi ya kisiasa.

62 Comments

  1. “Hey there. I found your website via Google at the same time as looking for a related matter, your website got here up. It seems to be good. I have bookmarked it in my google bookmarks to come back then.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*