Lubuva- Imarisheni utawala bora

jajiilubuva

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa utendaji wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.

Jaji mstaafu Lubuva ametoa mwito huo wakati akieleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya tume hiyo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi katika inatekeleza majukumu yake wakati huo, lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.

“Katika hali na mazingira ya Tume ya wakati huo, bila kusita nashawishika kusema kuwa Tume ya Kudumu ilianzishwa wakati ambapo si watu wengi kwa bahati mbaya Afrika ambao walijali haki za binadamu na utawala bora,” alisema Lubuva.

Aliongeza kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambao Tanzania ndio ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha TKU ili kunusuru wananchi kutakona na madhila ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.

“Kwa upande mwingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina kibarua kizito katika kutekeleza majukumu yake katika mazingira ya sasa ambapo tume hii si rahisi kuelezea kwa wananchi kwa nini isifanikiwe zaidi ya TKU,” alieleza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki alisema lengo kubwa la serikali kuanzisha TKU ilikuwa ni kumlinda mwananchi na lilifanikiwa kwa kushughulikia malalamiko 39,000 kwa kipindi cha miaka 35.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga alisema maadhimisho ya Miaka 50 ya TKU yamekwenda sambamba na kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kuanzisha tume hiyo, ikiwa ni taasisi ya kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma kwa wananchi.

Katika maadhimisho hayo, Mwalimu Nyerere na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi walipata Tuzo na Cheti cha kutambua mchango wao kuweka misingi ya uwajibika na utawala Bora.

70 Comments

  1. “Thanks , I’ve just been looking for information about this topic for a long time and yours is the best I have found out till now. But, what concerning the conclusion? Are you certain in regards to the source?”

  2. “It’s actually a nice and useful piece of information. I am satisfied that you simply shared this useful info with us. Please keep us up to date like this. Thank you for sharing.”

  3. “I have seen plenty of useful issues on your web-site about computers. However, I have got the thoughts and opinions that laptops are still more or less not powerful more than enough to be a good selection if you normally do tasks that require lots of power, for instance video editing. But for web surfing, word processing, and the majority of other prevalent computer functions they are just great, provided you do not mind small screen size. Many thanks for sharing your ideas.”

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*